Shirika la Blue Victoria lilibahatika kualikwa kwenye mjadala wa kitaifa wa siku mbili wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mjadala huu uliandaliwa na Wizara ya Nishati na kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan.
Katika mjadala huo shirika liliwakirishwa na Mkurugenzi wake Bwana Festus Massaho na alipata wasaa wa kuchangia.
"Ikiwa tunataka kutumia nishati safi ya kupikia, basi iendane na kubuni miundombinu inayoendana na kupika chakula chetu cha kitamaduni. Mfano ukitaka kupika ugali wa kula watu watano kwenye mtungi mdogo wa gesi si rahisi kama ukipikia kwenye mafiga matatu"..
Mkurugenzi Mtendaji wa Blue Victoria Bw Festus Massaho akiwa katika mdahalo wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia jijini Dar es Salaam.Shirika la Blue Victoria lilibahatika kualikwa kwenye mjadala wa kitaifa wa siku mbili wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mjadala huu uliandaliwa na Wizara ya Nishati na kufunguliwa na Rais wa JMT... pic.twitter.com/susFeOL81A
— Blue Victoria (@BlueVictoriatz) November 3, 2022